KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA WA MIFUPA, MAGONJWA YA NDANI NA NGOZI

TANGAZO HUDUMA ZA MADAKITARI BINGWA

Uongozi wa Hospitali ya Songambele iliyopo katika kijiji cha Nkololo wilaya ya Bariadi,

unapenda kuwatangazia wakazi wote wa Mkoa wa Simiyu na Viunga vyake, kuwa kutakuwa na kambi ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya kanda Bugando. Ambapo kutakuwa na Daktari Bingwa wa Mifupa, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ngozi kuanzia Tarehe 26/01/2026 hadi Tarehe 30/01/2026.

Huduma zitakazotolewa na Daktari Bingwa wa Mifupa:-

Matatizo ya Maumivu makali ya Mgongo, Nyonga, Miguu kuwaka Moto, Ganzi, maumivu ya jointi za Mifupa, matatizo ya mivunjiko mbalimbali iliyounga vibaya au iliyoshindikana kuunga, Miguu iliyopinda (Matege) na shida zote za mifupa.

Huduma zitakazotolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani:- Matatizo ya shinikizo la damu (Presha), kisukari, maumivu ya kifua na kukohoa kwa muda mrefu, shida ya mapafu, figo, vidonda vya tumbo, homa za mara kwa mara, mafuta mengi kwenye mishipa ya damu,, kizunguzungu, maumivu ya kichwa mara kwa mara, udhaifu wa mwili na mengine.

Huduma zitakazotolewa na Daktari Bingwa wa Ngozi

Matatizo ya nywele pamoja na kucha, vibarango, fangasi ya ngozi, chunusi au vipele visivyoisha, ngozi kuwasha, pumu ya ngozi kwa watoto, upele kwa watoto wadogo.

Pia huduma za Daktari bingwa wa magonjwa ya koo,pua, masikio, yanatolewa kila wiki siku ya Alhamisi.

Pia huduma za kila siku za Meno zinatolewa yaani Kutoa jino, Kuziba Jino, Kusafisha kinywa, Kupanga meno na kutibu harufu Mbaya Mdomoni.

HUDUMA ZITATOLEWA KWA MALIPO YA PAPO KWA PAPO, PAMOJA NA BIMA ZA NHIF NA BRITAM

MAWASILIANO-0686-031556

WOTE MNAKARIBISHWA SONGAMBELE HOSPITAL- NKOLOLO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *