TANGAZO HUDUMA ZA KIBINGWA
Uongozi wa Hospitali ya Songambele iliyopo katika kijiji cha Nkololo- Bariadi, unapenda kuwatangazia wakazi wote kuwa kutakuwa na ujio wa Madaktari Bingwa. Kutakuwa na Daktari Bingwa wa Mifupa, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani (Physician) na Daktari Bingwa wa Ngozi kuanzia tarehe 23/03/2026 hadi tarehe 27/03/2026.
Huduma zitakazotolewa kwenye klinic ya Magonjwa ya Mifupa:-
Matatizo ya Maumivu Makali ya Mgongo, Nyonga na Mifupa, Miguu kuwaka Moto, Ganzi, jointi za Mifupa, Matatizo ya mivunjiko mbalimbali iliyounga vibaya au iliyoshindikana kuunga, na Miguu iliyopinda (Matege).
Huduma zitakazotolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani ni:-
Magonjwa ya kisukari, Shinikizo la Damu (Presha), Magonjwa ya Moyo, Kiharusi (Stroke), Kifua kuuma au kubana (Pumu), Magonjwa ya Figo, Vidonda vya Tumbo, Pamoja na mengine mengi.
Huduma zitakazotolewa kwenye klinic ya Masikio, Koo na Pua ni kama zifuatazo:
Masikio kuuma na kutoka Usaha, Miungurumo masikioni na kutosikia, Koo kuuma, kushindwa au maumivu wakati wa kumeza, Mafua ya muda mrefu, Nyama za Puani zenye kusababisha kukoroma, kutokwa damu puani, Nyama za Kwenye Makoo (Tonsillitis), Vimbe za Shingoni (Goitre) na mengineyo.
Pia huduma za kila siku za Meno zinatolewa yaani Kutoa jino, Kuziba Jino, Kusafisha kinywa, Kupanga meno na kutibu harufu Mbaya Mdomoni.
HUDUMA ZITATOLEWA KWA MALIPO YA PAPO KWA PAPO, PAMOJA NA BIMA ZA NHIF NA BRITAM.
MAWASILIANO 0686-031556
USIKIAPO TANGAZO HILI MJULISHE NA MWENZAKO NYOTE MNAKARIBISHWA.
KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA NDANI, MIFUPA NA ENT(Sikio, Pua na Koo)











Leave a Reply