TANGAZO HUDUMA ZA KIBINGWA
Uongozi wa Hospitali ya Songambele iliyopo katika kijiji cha Nkololo-Bariadi, unapenda kuwatangazia wakazi wote kuwa kutakuwa na ujio wa Madaktari Bingwa. Kutakuwa na Daktari Bingwa wa Mifupa, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani (Physician) na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama kuanzia tarehe 20/04/2026 hadi tarehe 24/04/2026.
Huduma zitakazotolewa kwenye klinic ya Magonjwa ya Mifupa:-
Matatizo ya Maumivu Makali ya Mgongo, Nyonga na Mifupa, Miguu kuwaka Moto, Ganzi, jointi za Mifupa, Matatizo ya mivunjiko mbalimbali iliyounga vibaya au iliyoshindikana kuunga, na Miguu iliyopinda (Matege).
Huduma zitakazotolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani ni:-
Magonjwa ya kisukari, Shinikizo la Damu (Presha), Magonjwa ya Moyo, Kiharusi (Stroke), Kifua kuuma au kubana (Pumu), Magonjwa ya Figo, Vidonda vya Tumbo, Pamoja na mengine mengi.
Huduma zitakazotolewa kwenye klinic ya Mgonjwa ya Kinamama kama zifuatazo:
Matatizo ya uvimbe tumboni, kushindwa kushika au kubeba mimba, kuharibika kwa mimba, fangasi sehemu za siri, mpangilio mbovu wa hedhi, maumivu makali ya tumbo la chini yanayoambatana na kutoka uchafu sehemu za siri na mengine mengi.
Pia kuna huduma ya Daktari Bingwa wa Sikio, Pua na Masikio kila Wiki siku ya Alhamisi.
Huduma za kila siku za Meno zinatolewa yaani Kutoa jino, Kuziba Jino, Kusafisha kinywa, Kupanga meno na kutibu harufu Mbaya Mdomoni.
HUDUMA ZITATOLEWA KWA MALIPO YA PAPO KWA PAPO, PAMOJA NA BIMA ZA NHIF NA BRITAM.
MAWASILIANO 0686-031556
USIKIAPO TANGAZO HILI MJULISHE NA MWENZAKO NYOTE MNAKARIBISHWA.











Leave a Reply