KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA MIFUPA NA MAGONJWA YA NDANI

TANGAZO HUDUMA ZA KIBINGWA
Uongozi wa Hospitali ya Songambele iliyopo katika kijiji cha Nkololo- Bariadi, unapenda kuwatangazia wakazi wote kuwa kutakuwa na ujio wa Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Kanda Bugando. Kutakuwa na Daktari Bingwa wa Mifupa, na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani (Physician) kuanzia tarehe 23/11/2026 hadi tarehe 27/11/2026


Huduma zitakazotolewa kwenye klinic va Magonjwa ya Mifupa:-

Matatizo ya Maumivu Makali ya Mgongo, Nyonga na Mifupa, Miguu kuwaka Moto, Ganzi, jointi za Mifupa, Matatizo ya mivunjiko mbalimbali iliyounga vibaya au iliyoshindikana kuunga, na Miguu iliyopinda (Matege).


Huduma zitakazotolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani ni:-
Magonjwa ya kisukari, Shinikizo la Damu (Presha), Magonjwa ya Moyo, Kiharusi (Stroke), Kifua kuuma au kubana (Pumu), Magonjwa ya Figo, Vidonda vya Tumbo, Pamoja na mengine mengi.
Pia kuna huduma ya Daktari Bingwa wa Sikio, Pua na Masikio kila Wiki siku ya Alhamisi.
Huduma za kila siku za Meno zinatolewa yaani Kutoa jino, Kuziba Jino, Kusafisha kinywa, Kupanga meno na kutibu harufu Mbaya Mdomoni.
HUDUMA ZITATOLEWA KWA MALIPO YA PAPO KWA PAPO, PAMOJA NA BIMA ZA NHIF NA BRITAM.
MAWASILIANO 0686-031556
USIKIAPO TANGAZO HILI MJULISHE NA MWENZAKO NYOTE MNAKARIBISHWA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *